Abstract

Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchanganua mielekeo ya wanafunzi wa kozi za sayansi na Sanaa kuhusu ufundishaji wa Stadi za Mawasiliano kwa Kiswahili nchini Kenya. Mielekeo ni hisia walizonazo watu kuhusu jambo au kitu fulani na ni kigezo muhimu ambacho huathiri uitikiaji wa mtu husika. Aidha, kuchunguza visababishi vya mielekeo husika. Aidha, kuchunguza visababishi vya mielekeo husika na kubainisha maoni ya wakufunzi kuhusu umuhimu wa matumizi ya Kiswahili kufundishia stadi za mawasiliano. Muundo wa Uchunguzi Kimaelezo ulitumiwa, huku taasisi 5 za kiufundi za kitaifa na sampuli ya wanafunzi 148 wakishirikishwa katika utafiti. Fomula ya Balian (1988) ya uteuzi wa sampuli ilizingatiwa na ukusanyaji wa data ulitumia kitanga cha mielekeo ya hojaji ya Likert kilichokarabatiwa, maswali ya wazi na dodoso. Waaidha, Zanatepe ya Kichanganuzi Data ya Kitakwimu za Sayansi Jamii (SPSS) kilitumika kuchanganua data. Matokeo yalidhihirisha kuwa, asilimia 2.82 ya wanafunzi 142 waliohusishwa katika uchanganuzi walidhihirisha mielekeo hasi, ilhali asilimia 97.18 walionyesha mielekeo chanya kuhusu ufundishaji wa Stadi za mawasiliano kwa Kiswahili katika taasisi za kiufundi nchini Kenya. Aidha, wanafunzi wa kozi za Sanaa walidhihirisha mielekeo chanya ya chini wakilinganishwa na wenzao wa sayansi. Uchanya huu ulitokana na faida ya utoaji wa huduma uwandani kwa wateja wao waliyoiambatanisha na kuridhia Kiswahili kitumike katika ufundishaji wa stadi za mawasiliano. Matokeo ya utafiti huu ni ya umuhimu kwa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayanzi na Teknolojia na Taasisi ya Ukuzaji wa Mitaala, Kenya katika utungaji wa sera ya elimu katika taasisi husika.

Full Text
Paper version not known

Talk to us

Join us for a 30 min session where you can share your feedback and ask us any queries you have

Schedule a call

Disclaimer: All third-party content on this website/platform is and will remain the property of their respective owners and is provided on "as is" basis without any warranties, express or implied. Use of third-party content does not indicate any affiliation, sponsorship with or endorsement by them. Any references to third-party content is to identify the corresponding services and shall be considered fair use under The CopyrightLaw.