Abstract

Tafsiri ni taaluma kongwe ambayo imekuwa ikifanyika katika nyuga mbalimbali kama vile sheria, utabibu na lugha. Tafiti nyingi zimekitwa katika matatizo ya tafsiri kwa ujumla. Wataalamu wa tafsiri, hususani za kifasihi kama vile Mkinga (2005), Malangwa (2010) na Mekacha (2013), wametafiti kuhusu mbinu na matatizo ya kutafsiri matini za kifasihi. Data za makala hii zimetokana na mbinu ya uchambuzi wa matini na usaili. Wafasiri tofauti wametafsiri kazi za kifasihi kwa kuzingatia usanaa uliomo kwenye kazi husika. Makala hii inamulika tafsiri ya lugha ya ishara katika Wema Hawajazaliwa kwa kuzingatia mtazamo wa ulinganifu wa kimawasiliano. Wema Hawajazaliwa ni riwaya iliyotafsiriwa na Abdilatif Abdallah kutoka katika riwaya ya The Beautyful Ones are not Yet Born ya Ayi Kwei Armah. Makala hii iliongozwa na Nadharia ya Ulinganifu wa Kimawasiliano iliyoasisiwa na Nida (1964). Pamoja na wataalamu wengi kutafiti kuhusu matatizo ya tafsiri, bado tafsiri ya kifasihi haijafanyiwa tafiti za kutosha hususani katika lugha ya Kiswahili. Makala hii imebaini kuwa, mfasiri huzingatia lugha ya ishara katika tafsiri ya matukio mbalimbali ya kiishara.

Full Text
Paper version not known

Talk to us

Join us for a 30 min session where you can share your feedback and ask us any queries you have

Schedule a call

Disclaimer: All third-party content on this website/platform is and will remain the property of their respective owners and is provided on "as is" basis without any warranties, express or implied. Use of third-party content does not indicate any affiliation, sponsorship with or endorsement by them. Any references to third-party content is to identify the corresponding services and shall be considered fair use under The CopyrightLaw.