Abstract

Ikisiri Makala hii inaangazia historia ya maendeleo ya bonde la Kilombero na hasa, dira juu ya maendeleo ya bonde hili lililoko kusini-kati mwa Tanzania. Tangu kipindi cha mwanzo cha ukoloni, bonde lilisifiwa kuwa na rutuba ya kutosha na mipango mingi iliandaliwa kuitumia rutuba hiyo kwa uzalishaji mazao. Matumizi ya ardhi hii yalitarajiwa kuleta mageuzi makubwa vijijini na kuboresha maisha ya watu. Ili kuelewa vyema dhima na umuhimu wa mipango ya awali juu ya bonde la Kilombero, makala hii inaangazia historia ya maendeleo kupitia mipango ya siku za nyuma ili kuona namna mipango hiyo ilivyosaidia maendeleo ya sasa na siku zijazo. Dhamira kuu nne za historia ya maendeleo zimeainishwa na kujadiliwa. Dhamira hizo ni: uimarishaji wa kilimo; udhibiti wa ikolojia; miundombinu; na makazi. Makala hii inaleta mtazamo mpya kuhusu Kilombero, lakini mtazamo huo unaweza kutumiwa katika historia ya maendeleo ya mahali popote nchini Tanzania.

Full Text
Paper version not known

Talk to us

Join us for a 30 min session where you can share your feedback and ask us any queries you have

Schedule a call

Disclaimer: All third-party content on this website/platform is and will remain the property of their respective owners and is provided on "as is" basis without any warranties, express or implied. Use of third-party content does not indicate any affiliation, sponsorship with or endorsement by them. Any references to third-party content is to identify the corresponding services and shall be considered fair use under The CopyrightLaw.